Ijumaa, 9 Agosti 2013

VUTA HATUWA

Uje nikakuzawiji, nyumbani uwe siraji
Ndivyo ninavyotaraji,
Mpenzi,
Vuta hatuwa!

Uwe ukinipa maji, unipikie na uji
Kila ninapohitaji,
Mpenzi,
Vuta hatuwa!

Moyoni unifariji, uwe wangu mnoaji
Regina wangu mbuji,
Mpenzi,
Vuta hatuwa!

Ndoa yetu tudariji, ijapo sina mitaji
Mwenyezi ndiye Mpaji,
Mpenzi,
Vuta hatuwa!

(Kwa Huba Langu Laazizi, Regina Wango Muthelya, 2013).