Jumatatu, 19 Aprili 2021

MTAPITA MTIHANI!

Mie nina tabasamu, ilojikita usoni
Nilosubiri kwa hamu, kama ya mtu ndotoni
Siku iliyo muhimu, tuipokee nyoyoni
Kwa shangwe na kwa furaha, mtapita mtihani!
Kwa maneno ya adhimu, ya'mshayo tafrani
Alivyopanga Rahimu, mjua kesho ya nini
Ametupa na kalamu, tuandike mitihani
Kwa shangwe na kwa furaha, mtapita mtihani!
Maandao kemkemu, yamefanya tubaini
Na kuleta ufahamu, kwamba njia ni laini
Tena nyie marjamu, nafasi yenu si duni
Kwa shangwe na kwa furaha, mtapita mtihani!
GNPS idumu, iwashinde wapinzani
Tuandikishe takwimu, tusalie namba wani
Watahiniwa jikimu, imba tenzi za tenzi rohoni
Kwa shangwe na kwa furaha, mtapita mtihani!



Kwa ndugu zangu, wadogo wangu wote wapenzi wanaoifanya mitihani yao ya darasa la nane na kidato cha nne mwaka huu wa 2021, kwa niaba ya 2020, mwaka ule ulioathirika na tandavu la Ugonjwa wa Virusi vya Korona ulioripotiwa mwaka 2019 (UGOVIKO-19)