Jumapili, 4 Agosti 2013

ZIMWI

Linalokujuwa zimwi, ukakwisha halikuli
Kiu chake hakizimwi, kwa utamu wa asali!
Ada kwake haisomwi, majirani huwajali
Matajiri mashendea, upatapo wanalia!

Wakamsimanga tembo, na ukubwake wa kimo
Wajapotowa minyambo, mto chura sende mumo
Silaha sio misimbo, fanza mambo kwa kipimo
Mkongani kaingia, mwisho tembo lililia!

Wa sitara hasumbuki, japokosa maakuli
Asumbuka mwenze chuki, wa moja havai mbili
Juwa baada ya dhiki, na faraja huwasili
Shetani hunyong'onyea, goti Mola kipigia!

Maoni 1 :

  1. SHUJAA SIMMANYI

    Namtafuta mmoya, mwenye kwelewa misimbo
    Kunga mwenye kusikiya, naye tukanene yambo
    Kama ni nyama kufiya, tufunge pasi yigambo
    Kwa busara za mafumbo, tukashauri umati

    JibuFuta