Nina hasira moyoni, nimeshindwa vumiliya!
Namsaili Manani, satuwa kusubiriya
Visa tuliona Pwani, kamwe visijerudiya!
Mbwa-mtu tangu lini, "mapenzi" kuyadoweya?
Kaja huyo Baniani, mapeni kuwapatiya
Na kamera mkononi, mbwa kamfunguliya!
Mabinti zetu jamani, mbona soni mwajitiya?
Mbwa-mtu tangu lini, "mahaba" kuyatezeya?
'Wapenzi' niambiyani, nisije potoka njiya
Mbona tumejilaani, kwa nyendo zilopoteya?
Hii sasa Kenya gani, mahoka twajitupiya?
Mbwa-mtu tangu lini, "ngono" wakafurahiya?
Nema mbiu napigani, naomba mnisikiya!
Mili yetu ya thamani, maradhi jiepushiya!
Mabinti nanyi mabini, rekebisheni tabiya!
Mbwa-mtu tangu lini, kitanda kujilaliya?
Nimefurahi wendani, kwa hili kulitangiya
Sote tukaunganeni, tuipige vita haya!
'Tendo la uhayawani, unajisi latutiya:
Mbwa-mtu tangu lini, nikaha kushirikiya?
Glen umebusuri, ni bora huyo wa Nyeri
Mie naona ni heri, ameikata dhakari!
Kilema uwe vizuri, mzima uchomwe nari!
Mbwa-mtu tangu lini, sahani moja kuliya?
Namunukuu Karima, kwa neno la Bibliya:
"Ni bora uwe kilema, mbinguni ukaingiya
Kuliko kuwa mzima, Jehannum kupoteya!"
Mbwa-mtu tangu lini, kudongozaniya njiya?
YETU MACHO
JibuFutaNashangaa nashangaa, mabinti wa dotikomu!
Dijito imewatwaa, wamsahau Rahimu
Mapenzi wayagawaa, bora wanazo kondomu
Kweli dunia shujaa, imeshinda waalimu!